Wizara ya Michezo kukuza vipaji mashinani, asema Tum

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya Michezo itashirikiana na kaunti ya Machakos katika utambuaji na ukuzaji vipaji vya michezo miongoni mwa vijana kutoka mashinani.

Haya yalisemwa jana na Katibu katika Wizara ya Michezo Mhandisi Peter Tum alipohudhuria fainali ya soka kati ya wanahabari wa Machakos na wenzao wa Nairobi katika uwanja wa Kenyatta, kaunti ya Machakos siku ya Alhamisi.

Katibu wa Wizara ya Michezo Mhandisi Peter Tum alipomtembelea Gavana wa Machakos, Wavinya Ndeti

Tum aliandamana Katibu katika Wizara ya Utekelezaji na Usimamizi Veronica Nduva.

Mechi hiyo ililenga kuangazia uhamasishaji na kukomesha dhuluma za kijinsia na kumaliza unyanyapaa wa dhuluma hizo kupitia vyombo vya habari.

Tum kifuatilia mechi

Tum aliyeandamana na mwenyeji wake, Gavana wa kaunti ya Machakos, Wavinya Ndeti alitoa zawadi za mipira na shilingi laki moja na kombe kwa wanahabari wa Machakos walioibuka na ushindi wa mabao 11 kwa bila.

  1. Katibu Tum akikabidhi zawadi kwa washindi

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wengine wa kaunti hiyo akiwemo Waziri wa Michezo Peter Kilonzo.

Share This Article