Wizara ya Leba na ulinzi wa jamii itaandaa usaili wa wakazi 1,000 wa kaunti ya Nakuru wanaopania kufanya kazi ughabini.
Waziri wa Leba Alfred Mutua ametangaza kuwa usaili huo utaandaliwa kesho kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moija jioni katika chuo Rift Valley National Polyethnic, .
Zoezi hilo linafutia kukamilika kwa usajili mwingine katika kaunti za Machakos,Makueni na Kitui.
Watakaopasi mahoajiano hayo watapata fursa ya kufanya kazi katika mataifa ya Australia, Qatar, Poland, Dubai, Saudi Arabia na Ujerumani miongoni mwa mataifa mengine.
Mutua amewataka watakaohudhuria zoezi hilo kesho kubeba stakabadhi za za kujitambukiusha na vyeti vya elimu.
Wakenya 3,247 walisajiliwa katika awamu ya kwanza huku nusu yao wakiwa tayari wamepata vyeti vya kusafiriki kuenda kuafanya kazi.