Sekta ya kilimo yatengewa shilingi bilioni 54.6

Martin Mwanje
1 Min Read

Sekta ya kilimo imetengewa jumla ya shilingi bilioni 54.6 katika bajeti ya mwaka 2024/2025. 

Akizungumza wakati akisoma bajeti hiyo katika bunge la taifa leo Alhamisi, Waziri wa Fedha Prof. Njuguna Ndung’u amesema fedha hizo ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuhakikisha nchi hii ina usalama wa chakula na lishe.

Kati fedha hizo, shilingi bilioni 10 zimetengewa mpango wa utoaji mbolea ya ruzuku kwa wakulima huku shilingi bilioni 6.1 zikitengewa mradi wa kitaifa wa kilimo wa maendeleo ya uongezeaji thamani.

Kwa upande mwingine, shilingi bilioni 2.5 zitatumiwa kukabiliana na nzige kwa dharura huku shilingi bilioni 2.4 zikitumiwa kuwawezesha vijana na wanawake katika kilimo.

Shilingi milioni 642.5 zitatumiwa katika mradi wa usalama wa chakula na kuhakikisha uwepo wa mimea mbalimbali.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *