Wizara ya elimu imetoa shilingi bilioni 6 nukta 2 kwa shule zote za umma nchini huku pesa hizo zikitarajiwa kufika kwa akaunti za shule ifikiapo Jumaytano ijayo.
Katika wizara ya Elimu Belio Kipsanh ametoa taarifa Ijumaa jioni akisema kuwa pesa hizo zitagharamia shule za umma za junior na zile za upili.
Kati ya kiwango hicho shule za Junior secondary zimetengewa shilingi bilioni 1 nukta 7 shule za msingi za umma shilingi bilioni 1 nukta 5 na shule za Free Day Secondary zikitengewa shilingi bilioni 12 nukta 9.
Shuke zote zilifungua kwa muhula wa tatu Agosti 28 mwaka huu ambao uantarajiwa kukamilika Oktoba 27 kabla ya kupisha mitihani ya kitaifa.
Kulinga na Kipsang pesa zilizotolewa Ijumaa ni sehemu ya shilingi bilioni 89 nukta 4 ambazo zilitengewa shule mwaka 2022-2023.