Wizara ya elimu yatoa ripoti ya ufadhili wa masomo

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu.

Wizara ya Elimu imetoa ripoti ya ufadhili wa masomo nchini mwaka 2023, katika viwango mbalimbali vya masomo.

Ripoti hiyo iliyotolewa na waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, imefafanua kuwa shilingi bilioni 67 kwa masomo ya shule za msingi na za sekondari za umma tangu mwezi Januari mwaka huu.

Kiwango hicho kinajumuisha shilingi bilioni 7 nukta 9 kwa wanafunzi milioni 9 wa shule za msingi za umma,shilingi bilioni 14 nukta 7, kwa wanafunzi milioni milioni 1 wa Junior Secondary na bilioni 44 nukta 4 zimetolewa kugharamia masomo ya bure kwa shule za kutwa za sekondari.

kwa wanafunzi wanaondelea na masomo ya vyuo vikuu na vya kiufundi , shilingi bilioni 51 nukta 1 zimetolewa tangu Januari,wengi wao wakiwa wa mwaka wa masomo 2023/2024.

Kufikia Oktoba 4 mwaka huu halmashauri ya Elimu ya juu HELB,ilitoa shilingi bilioni 10 nukta 5 kugharamia masomo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo.

Waziri Machogu amewataka wasimamizi wa vyuo vikuu na vile vya kiufundi kuwaruhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuendelea na masomo, huku bodi ya HELB ikiendelea na mchakato wa kutayarisha mikopo yao na kuwataka wanafunzi ambao hawajatuma maombi ya mikopo hiyo kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.

TAGGED:
Share This Article