Katibu wa elimu ya msingi Belio Kipsang ametangaza kuwa wizara ya elimu inapania kujenga madarasa 16,000, kwa kundi la kwanza la wanafunzi wa gredi ya 9 mwaka ujao.
Kipsang ameongeza kuwa madarasa hayo yatakuwa tayari ifikiapo Januari mwaka 2025.
Katibu huyo ameongeza kuwa wizara yake itawaajiri walimu 20,000 wapya mwaka ujao kupiga jeki mtaala wa elimu ya umilisi CBC