Wizara ya Afya Ukanda wa Gaza yasema watu zaidi ya 42,000 wameuawa vitani

Martin Mwanje
0 Min Read

Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza inasema watu wasiopungua 42,010 wamefariki katika vita vinavyoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina.

Idadi hiyo inajumuisha vifo 45 vilivyotokea saa 24 zilizopita.

Wizara hiyo inasema watu 97,720 wamejeruhiwa katika ukanda huo tangu kuanza kwa vita hivyo.

Vita hivyo vilianza wakati wanamgambo wa Hamas walipofanya mashambulizi nchini Israel Oktoba 7, 2023.

Share This Article