Wizara ya Afya katika eneo la Gaza imesema kuwa watu wasiopungua 41,788 wameuawa kutokana na vita kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina.
Vita vimekuwa vikiendelea eneo hilo linaloongozwa na kundi la Hamas kwa muda wa miezi 12 sasa.
Idadi ya waliofariki inajumuisha vifo 99 vilivyotokea katika muda wa saa 24 zilizopita, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza.
Imeongeza kuwa watu 96,794 wamejeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita hivyo Oktoba 7 mwaka jana.
Vita hivyo vilianza baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel.