WHO: Mapigano yanahujumu juhudi za kuangamiza Ebola DRC

Ghebreyesus, alisema mapigano karibu na hospitali kwenye mkoa wa Ituri, yalivuruga juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.

Tom Mathinji
1 Min Read
Tedros Adhanom Ghebreyesus - Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus, ametoa wito wa kudumishwa kwa amani katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambalo ni kitovu cha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Ghebreyesus, alisema mapigano karibu na hospitali kwenye mkoa wa Ituri, yalivuruga juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, huku wahudumu wa afya walikazimika kutafuta hifadhi kwenye wodi moja ya kujifungulia kina mama kwa zaidi ya saa 24.

“Mapigano makali yamekuwa yakiendelea kwenye eneo la hospitali katika mkoa wa Ituri, ambako mlipuko wa kwanza wa ugonjwa wa Ebola uliibuka,” Tedros kwenye ukurasa wa  X.

Kulingana na mkurugenzi huyo, mapigano hayo yamesambaratisha juhudi za hospitali hiyo kukabiliana na Ebola, na kuwakeka wagonjwa, wahudumu wa afya na familia kwenye hatari kubwa.

Alisema  WHO  inatafuta mbinu za kuwahamisha wahudumu hao wa afya hadi katika maeneo salama.

“Dawa bora ni upatikanaji amani,” aliongeza Mkurugenzi huyo.

Kufikia tarehe 17 mwezi Novemba, WHO ilinakili vifo  5,678 kutokana na makali ya Ebola nchini DRC, hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi kunakiliwa nchini humo.

Share This Article