Wezi waliokuwa wamejihami wanaripotiwa kuvamia bweni moja la wanafunzi wa kike katika chuo kikuu cha Ibadan jimbo la Oyo nchini Nigeria, alfajiri ya Jumamosi Februari 15, 2025.
Wanadaiwa kupokonya wanafunzi waliokuwepo kwenye bweni la Awolowo mali zao huku wakidhulumu wengine katika shambulizi hilo lililodumu masaa kadhaa. Wanafunzi waliripoti kuibiwa simu, nguo na vitu vingine vya thamani.
Kufuatia kamsa za mabinti hao, baadhi ya wezi walikamatwa na kukabidhiwa maafisa wa polisi, katika kituo cha polisi cha Sango.
Maafisa wa usalama katika eneo hilo wameanzisha msako kwa nia ya kukamata wezi wengine ambao walifanikiwa kutoroka.
Msemaji wa chuo hicho cha Ibadan kwa jina Joke Akinpelu alithibitisha kisa hicho alipohutubia wanahabari.
Tukio hili linajiri miezi mitatu tu baada ya chuo hicho kuorodheshwa kati ya taasisi zenye hatari kubwa ya ufisadi na tume huru ya kupambana na ufisadi na makosa mengine.