Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula ameliomba shirika la umoja wa kimataifa kuhusu haki za watoto (UNICEF), kuwapa kipa umbele watoto wa kiume katika miradi yake ya kupigania haki za watoti.
Wetang’ula amehoji kuwa mashirika mengi yanaangazia zaidi haki za mtoto wa kike na kumwacha wa kiume hatarini .
“Mtoto wa kioume nchini anaumia kimyakimya bikla kuzungumza .Juhudi zote zimeelekezwa katika kumpigania na kumuinua msichana.UNICEF wana uwezo na wanapaswa kuingia kati kubadilisha hali.”akasema Wetang’ua
Wetang’ula amesema haya Alhamisi alipotembelewa na mwakilishi wa UNICEF, nchini Kenya Dr Shaheen Nilofer, aliyemtembelea katika majengo ya bunge.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na naibu Spika Gladys Boss na mwakilishi wa akina mama kutoka kaunti ya Homabay Fatuma Zainab.
UNICEF iliahidi kuendelea kuunga mkono miradi kadhaa ya maendeleo nchini ikiwemo katika sekta za elimu,kilimo na ulinzi wa wakongwe.