Wenyeji Australia waiparuza Denmark na kufuzu robo fainali ya Kombe la Dunia kwa wanawake

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji Australia wamejikatia tiketi kwa robo fainali ya Kombe la Dunia kwa wanawake baada ya kuwalaza Denmark magoli mawili kwa bila katika mechi ya raundi ya 16 bora, iliyosakatwa katika uwanja wa Olympic mjini Sydney leo Jumatatu adhuhuri.

Caitlin Foord alipachika bao la kwanza kwa wenyeji Matildas katika dakika ya 29 kabla ya Hayley Raso kutanua uongozi kwa bao la dakika ya 70.

Australia watapambana na mshindi kati ya Morocco na Ufaransa katika kwota fainali.

Ratiba iliyobainika ya kwota fainali ni kati ya Uhispania na Uholanzi na ile kati ya Japani na Uswidi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *