Wengine watano wafariki kwa utapiamlo Gaza saa 24 zilizopita

Martin Mwanje & BBC
1 Min Read
Hamza Mishmish, 25, huko Gaza anaonyesha dalili za utapiamlo katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat huku kukiwa na njaa. Picha hii ilipigwa Julai 27. / Picha kwa hisani ya BBC

Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, watu watano wamefariki kutokana na utapiamlo, kulingana na taarifa ya hivi punde kutoka kwa Wizara ya Afya inayoendeshwa na kundi la Hamas.

Hiyo inaifanya jumla ya vifo vya utapiamlo kufikia 222, inasema wizara hiyo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu lilisema siku ya Ijumaa kwamba kiasi cha misaada inayoingia Gaza kinaendelea kuwa “chini ya kiwango kinachohitajika kukidhi mahitaji makubwa ya watu.”

Israel imekanusha kuwa kuna njaa huko Gaza na kuyashutumu mashirika ya Umoja wa Mataifa, UN kwa kutochukua misaada katika mipaka na kuipeleka Gaza.

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu linasema linaendelea kuona vikwazo na ucheleweshaji wakati likijaribu kukusanya misaada kutoka maeneo ya mpaka yanayodhibitiwa na Israel.

Wakati huo huo,Wizara hiyo imetoa taarifa ikisema watu 69 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hiyo inaifanya idadi ya Wapalestina waliouawa tangu kuanza kwa vita kufikia 61,499, huku zaidi ya watu 150,000 wakijeruhiwa, kulingana na wizara hiyo.

Martin Mwanje & BBC
+ posts
TAGGED:
Share This Article