Wazito FC imesalia ligini msimu ujao baada ya kuwashinda Migori Youth, mabao matatu kwa bila katika mechi ya mchujo iliyosakatwa Jumamosi katika uwanja wa Muhoroni.
Wazito ilimali ya 16 ligini msimu uliopita huku Muhoroni wakimaliza katika nafasi ya tatu katika ligi ya daraja ya kwanza NSL .
Stephen Mbulere alipachika goli la kwanza kupitia mkwaju wa adhabu muda mfupi kabla ya mapumziko kabla ya Robert Onyango kuongeza la pili mwanzoni mwa kipindi cha pili huku Collins Neto akitanua uongozi kwa bao la tatu.
Wazito FC watafungua msimu mpya wa ligi kuu ya FKF msimu wa mwaka 2023 na 2024 dhidi ya Nairobi City Stars Agosti 27, 2023.