Waziri wa zamani wa Utalii Najib Balala alikamatwa Alhamisi usiku na katibu wake wa zamani Leah Adda Gwiyo kutoka nyumbani kwao.
Balala na katibu wake wa zamani,na afisa wa kampuni ya West Consult Engineers Joseph Odero, walikamatwa na maafisa wa tume ya maadili na kupambana dhidi ya ufisadi EACC.
Watatu hao wanakabiliwa na mashtaka ya kulipa shilingi bilioni 8.5 kwa ujenzi wa chuo cha Utalii ambacho kwa sasa kinajulikana kama Ronald Ngala Utalii College,eneo la pwani
Kulingana na EACC Balala alikuwa asafirishwe kwa ndege kutoka Nairobi hadi Mombasa na baadaye kufukishwa katika mahakama ya Malindi.