Waziri wa Utalii na Urithi wa Zanzibar Simai Mohamed Said amejiuzulu kwa madai ya mazingira yasiyopendeza ya kazi.
Katika taarifa, Said alisema aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais wa visiwa vya Zanzibar Hussein Mwinyi siku ya Alhamisi.
“Nimefanya uamuzi huu mgumu, ambao si rahisi katika utamaduni wetu,” aliongeza.
“Nitaendelea kuwa mwaminifu kwa serikali na chama changu cha Mapinduzi.
Charles Hillary, msemaji wa rais katika visiwa hivyo , amethibitisha kujiuzulu kwa waziri huyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.
Kujiuzulu kwake kumekuja siku chache baada ya kuripotiwa kulalamikia uhaba wa pombe Zanzibar akisema unaathiri sekta ya utalii.
Takriban asilimia 90 ya uchumi wa Zanzibar hutegemea utalii.