Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan aonya mashambulizi ya Israel yanaweza yakasababisha ‘vita kamili vya kikanda’

Martin Mwanje
1 Min Read
Ayman Safadi - Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi leo Jumatatu ameonya kuwa “mashambulizi ya Israel” yanalisukuma eneo hilo kuelekea “lindi kuu” la mapigano kamili.

Safadi alikuwa akizungumza wakati wa ziara yake nchini Lebanon ambako Israel inasema inafanya mashambulizi yanayolenga maeneo ya wanamgambo wa Hezbollah.

“Mashambulizi ya Israel… yaliyoanza katika eneo la Gaza na sasa yameendelea hadi Lebanon yanalisukuma eneo lote katika lindi kuu la vita kamili vya kikanda,” Safadi ameuambia mkutano wa wanahabari mjini Beirut.

Website |  + posts
Share This Article