Waziri wa Afya Susan Nakhumicha aapa kumaliza ufisadi KEMSA

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri wa Afya Susan Susan Nakhumicha aameapa kumaliza ufisadi katika shirika la kusambaza dawa na vifaa vya matibabu nchini KEMSA na hazina ya kitaifa ya bima ya matibabu NHIF.

Anasema amejitolea kukabiliana na makundi ya ufisadi yenye ushawishi mkubwa katika shirika la KEMSA na wizara kwa jumla ambao wanashirikiana na wafanyakazi wafisadi wa serikali ili kukomesha uovu huo katika mashirika hayo mawili makubwa nchini.

Nakhumicha aliyasema hayo akiwa huko Kitale ambako aliongoza hafla ya kupandishwa hadhi kwa hospitali ya St. John’s Mission kutoka level 3 hadi level 4. Alihakikishia wasimamizi wa hospitali hiyo uungwaji mkono kutoka kwa serikali.
Alitoa mchango wa madawa ya thamani ya shilingi laki tatu kwa hospitali hiyo.

Shirika la KEMSA linakabiliwa na kashfa ya mabilioni ya pesa ambayo ilisababisha hazina ya Global Fund kutupilia mbali zabuni ya shilingi bilioni 3.7 ya neti za kuzuia mbu zilizotiwa dawa baada ya ripoti kuchipuza kwamba kampuni moja ya Uchina ambayo iliafiki mahitaji yote ya kupata zabuni hiyo ilizuiwa kuwania zabuni hiyo.

Hazina ya the NHIF, nayo inakumbwa na madai kwamba maafisa wake wamekuwa wakishirikiana na hospitali kadhaa kupora pesa za hazina hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *