Waziri Owalo aituza Gor Mahia shilingi milioni 2 kwa kushinda ligi

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Habari na Mawasiliano Eliud Owalo amewatuza mabingwa wa ligi kuu Gor Mahia shilingi milioni 2 huku akiwapa changamoto ya kusajili matokeo bora barani Afrika.

Owalo alisema haya Jumatatu alipoandaa dhifa ya chakula cha mchana kwa timu hiyo baada ya kunyakua taji la 21 la ligi kuu siku ya Jumapili.

Waziri pia aliwashauri wachezaji wa timu hiyo kusalia kikosini kwa muda mrefu ili kuafikia matokeo bora.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na maafisa wakuu wa timu hiyo akiwemo aliyekuwa kocha Jonathan McKingstry na mweyekiti Ambrose Rachier miongoni mwa wengine.

Website |  + posts
Share This Article