Waziri Owalo aitunuku Gor Mahia basi jipya la shilingi milioni 20

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Eliud Owalo, amewakabidhi mabingwa wa ligi kuu Gor Mahia basi jipya la kima cha shilingi milioni 20 katika sherehe ya kufana iliyoandaliwa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani mapema Jumamosi.

Waziri Owalo akihutubia halfa hiyo, amekariri kujitolea kuisaidia klabu hiyo kujenga uwanja wao na pia kuwa na jumba lao kama njia moja ya kuipandisha hadhi kufikia viwango vya timu nyingine maarufu Afrika.

Owalo pia ameipa changamoto timu hiyo kuhifadhi taji ya ligi kuu msimu huu wakishikilia nafasi ya pili kwa pointi 20.

Halfa hiyo ilihudhuriwa na katibu katika Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano anayesimamia utangazaji Professa Edward Kisiangani,Mbunge wa Kasarani Ronald Karauri na viongozi wa timu .

Waziri Owalo na Katibu wake Edward Kisiangani

Waziri Owalo pia aliitunuku klabu hiyo shilingi milioni 3 msimu uliopita waliponyakua ubingwa wa ligi kuu,wakati ambapo hakukuwa na zawadi ya pesa kwa washindi wa ligi kutoka kwa shirikisho la soak nchini FKF.

Gor Mahia maarufu kama K’ogalo itakabiliana na Murang’a Seal katika mchuano wa Jumamosi Alasiri.

Website |  + posts
Share This Article