Waziri wa Elimu Julius Ogamba anatarajiwa kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, KCSE, ya mwaka 2024 leo Alhamisi.
Waziri anatarajiwa kutangaza matokeo hayo katika jumba la Mtihani wakati wowote kuanzia sasa.
Ogamba alimtaarifu Rais William Ruto juu ya matokeo hayo mapema leo Alhamisi.
Matokeo hayo kwa kawaida hutangazwa mwezi Disemba lakini wakati huu yamekawia mno na kuwatia hofu watahiniwa.
Yamkini yalicheleweshwa kwa lengo la kuyahakiki vyema na kuepusha kasoro zilizoshuhudiwa wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya mwaka 2023.
Watahiniwa 962,512 walikalia mtihani wa KCSE mwaka jana.