Waziri Mvurya akutana na wawezekaji wa kibinafsi kuhusu CHAN

Waziri aliwataka wawekezaji hao kutumia fursa ya kipekee iliyopo ya CHAN kujiimarisha na pia kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Michezo Salim Mvurya amekutana na wawekezaji kutoka sekta za kibinafsi (KEPSA) kuzungumzia fursa zilizopo kwenye fainali za kombe la CHAN zitatakazoandaliwa kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu.

Waziri aliwataka wawekezaji hao kutumia fursa ya kipekee iliyopo ya CHAN kujiimarisha na pia kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mvurya aliandamana na katibu wake, Elijah Mwangi, na mwenyekiti wa kamati andalizi ya CHAN, Nicholas Musonye.

Kenya itaandaa mechi za kundi A katika viwanja vya Kasarani na Nyayo huku fainali ikisakatwa ugani Kasarani Agosti 30.

Jumla ya mataifa 19 yatashiriki fainali hizo ambazo zitaandaliwa kwa pamoja na Kenya,Uganda,Tanzania na Zanzibar.

 

Website |  + posts
Share This Article