Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech Prof. Petr Fiala amewasili humu nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu.
Punde alipowasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta, Prof. Fiala alilakiwa na Waziri mwenye Mamlaka Makuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi.
Wakati wa ziara hiyo, Prof. Fiala atafanya mazungumzo na maafisa waandamizi serikalini na wale wa sekta mbalimbali.
Waziri huyo Mkuu wa Czech amepangiwa kukutana na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi kesho Jumanne.
Ziara ya Prof. Fiala inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Jamhuri ya Czech katika nyanja mbalimbali.
Aidha makubaliano kadhaa ya pande mbili yanatarajiwa kutiwa saini kati ya mataifa hayo wakati wa ziara hiyo.