Waziri Mkuu wa DRC Jean-Michel Sama Lukonde ajiuzulu

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mkuu DRC Sama Lukonde.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Michel Sama Lukonde amejiuzulu, ametangaza hatua hiyo katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ya ofisi ya rais Jumanne jioni.

Rais Felix Tshisekedi alikubali kujiuzulu kwa Bw Lukonde, shirika la habari la Reuters liliripoti, likitoa taarifa kutoka kwa ofisi ya rais.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Rais Tshisekedi aliiomba serikali ya Bw Lukonde kuendelea na majukumu yake hadi serikali mpya itakapoundwa.

Nchini DRC, serikali inaongozwa na waziri mkuu.

Lukonde sasa ataanza kazi ya kuwa mbunge, baada ya kupigiwa kura bungeni katika uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi Disemba mwaka jana.

Lukonde alikuwa ameteuliwa kuwa waziri mkuu mwaka wa 2021, akimrithi aliyekuwa Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba, ambaye alijiuzulu baada ya wabunge kupitisha kura ya kutokuwa na imani naye na serikali yake.

Share This Article