Waziri wa Utalii na Wanyamapori Rebecca Miano amekanusha madai yanayozagaa mitandaoni kuhusu kushambuliwa kwake mapema Jumatatu akielekea afisini.
Madai hao yaliashiria kuwa Waziri huyo alishambuliwa na wahuni mapema leo Jumatatu.
Kwenye taarifa, Miano ametaja madai hayo kuwa porojo na yasiyo na msingi akisema yuko katika hali shwari ya kiafya na anatekeleza majukumu yake kama kawaida.
Waziri amekashifu vikali madai hayo akitaka umma kuthibitisha taarifa zozote kutoka kwa Wizara yake badala ya kupotoshwa.
Wiki iliyopita, msemaji wa serikali Charles Owino alionya kuwa uhuni na taarifa za upotoshaji vinaweza kuwa tishio kwa umoja wa taifa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 20227.