Waziri wa Uchumi wa Baharini na masuala ya usafiri wa majini Hassan Joho, alifanya kikao na Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman, siku ya Jumatano katika ofisi ya waziri huyo jijini Nairobi.
Joho na Bi Whitman walijadiliana kwa mapana kuhusu ushirikiano wa Kenya na Marekani, hususan katika masuala ya uwekezaji katika sekta za uchimbaji madini, uchumi wa baharani na usafiri wa majini.
Wawili hao walijadiliana kuhusu ushirikiano utakaokuza uchumi wa Kenya na kubuni nafasi za ajira kwa vijana.
Ushirikiano hupo unalenga kuimarisha kuongeza tija kwa madini yanayopatikana katika nchi hizo mbili ,kuimarsha uwekezaji katika uchumi wa baharini katika sekta kama vile; uhifadhi wa samaki kwa kutumia barafu,ufugaji samaki na kuimarisha usalama wa usafiri wa majini.
Makatibu wandamizi katika wizara ya Madini Elijah Mwangi, mwenzake kutoka wizara ya madini Bi Betsy Njagi katibu wa Wizara usafiri wa majini Geoffrey Eyanae Kaituko kutoka Idara ya usafiri wa majini na meli walihudhuria mkutano huo.