Waziri Eluid Owalo aongoza upanzi wa miti Nandi

Rahab Moraa
1 Min Read

Jumla ya miti zaidi ya miche 8,000 imepandwa katika eneo la Karimarich, kaunti ya Nandi na timu iliyoongozwa na waziri wa habari, mawasiliano na uchumi wa dijitali Eliud Owalo.

Timu hiyo ilijumuisha maafisa wa serikali na wanajamii kufanikisha sehemu ya mpango wa serikali ya upanzi wa miti bilioni 15.

Owalo alieleza umuhimu wa kupanda miti haswa wakati wa mvua kama njia inayowezekana ya kuhifadhi mazingira na kusaidia kilimo endelevu.

Alihimiza wakenya kushiriki katika upandaji miti kote nchini, akibainisha kuwa pia ni chanzo cha mapato katika eneo la mikopo ya kaboni.

Rahab Moraa
+ posts
Share This Article