Waziri Ababu azuru Kisumu kukagua ujenzi wa uga wa Moi

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba siku Ijumaa amezuru uwanja wa Moi katika kaunti ya Kisumu, kufanya ukaguzi wa ukarabati wake kwa maandalizi ya michuano ya CECAFA kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18.

Waziri Ababu amekariri kujitolea kwa serikali ya kitaifa kuboresha miundo mbinu ya michezo nchini.

Haya yanajiri huku Kenya ikijukumiwa kuandaa mashindano ya kombe la CHAN Septemba mwaka ujao na fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2027.

Waziri Ababu ipokelewa na mwenyeji wake Gavana wa kaunti ya Kisumu Professa Anyang’ Nyong’o.

Kaunti mbalimbali nchini zimeonyesha ari kuataka kuandaa mechi za kombe la CHAN na pia AFCON.

Share This Article