Waziri wa Michezo Ababu Namwamba ameteuliwa katika jopo la mawaziri wa Jumuiya ya Madola wanaohusika na masuala ya vijana kwa kipindi cha miaka minne.
Uteuzi huo ulifanyika jijini London nchini Uingereza jana Alhamisi usiku ambako Namwamba alihudhuria kongamano la kumi la kimataifa la Jumuiya ya Madola.
Nafasi ya Namwamba katika jumuiya hiyo itasaidia katika kuwasilisha ajenda ya vijana wa Kenya kwa mataifa 56 wanachama wa Jumuiya ya Madola.