Wazee zaidi ya 400 katika kaunti ndogo ya Kiambu Mjini wamesajiliwa katika bima ya afya ya NHIF kupitia ufadhili wa pesa za kustawisha eneo bunge, NG-CDF.
Akizungumza wakati wa usajili huo, mbunge wa Kiambu Mjini Machua Waithaka alisema kuwa watatumia pesa shilingi milioni 3 kuwasajili wanufaika wa kwanza ambapo wanatarajia kuwasajili zaidi ya watu 1,000.
Mbunge huyo alisema kuwa mpango wa bima ya NHIF utahakikisha kuwa zaidi ya wazee na walemavu 500 watanufaika katika eneo lake la bunge ili waweze kupata huduma za afya bila mzigo wowote.
Walionufaika walionyesha furaha yao na kusema wamekuwa wakipitia changamoto nyingi zikiwamo kukosa kulipia ada za NHIF hivyo basi kutopata huduma za matibabu.