Wazazi watakiwa kuwashauri watoto wao wasipotoke

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu wa wizara ya Usalama wa Taifa, Dkt. Raymond Omollo.

Serikali imetoa wito kwa wazazi na wazee kuwashauri vijana dhidi ya fujo.Katibu katika wizara ya usalama wa kitaifa Dkt. Raymond Omollo, ametoa wito kwa wazee katika jamii kujihusisha zaidi katika maisha ya vijana na kuwasaidia kuwa watu wenye maadili mema ambao wanaheshimu taasisi na mifumo ambayo ni msingi wa maadili ya kidemokrasia.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa tarafa za Mutarakwa na Kapletundo kwenye kaunti ya Bomet , Dr. Omollo alikashifu visa vya ghasia na makabiliano na polisi pamoja na uporaji wa mali ,akionya kuwa wote waliohusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Alisema ghasia zilizoshuhudiwa hivi majuzi ziliathiri pakubwa maadili ya kidemokrasia nchini huku akiwahimiza wanasiasa dhidi ya kuwatumia vibaya vijana kuvuruga amani nchini.

“Tuwashauri watoto wetu wasipotoke. Kenya ni nchi inayoongozwa na sheria. ikiwa una shida na viongozi wa sasa, unafursa ya kufanya mabadiliko kupitia uchaguzi,” alisema Omollo.

Alitoa wito kwa wabunge kufanyia marekebisho sehemu ya 37 ya katiba ili kutoa fursa kwa maandamano ya amani na kuzuia mwingilio wa wahalifu wanaosababisha uharibifu na wizi.

Website |  + posts
Share This Article