Wazazi wataka sheria ya kupambana na mihadarati kupitishwa haraka

Carolyn Necheza
1 Min Read

Muungano wa Kitaifa wa Wazazi umeitaka serikali kupitisha haraka sheria dhidi ya matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya shuleni, baada ya ripoti ya Mamlaka ya Kitaifa ya Kupambana na Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya (NACADA) kuonyesha ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi na walimu.

Wakizungumza mjini Kakamega katika warsha ya siku tatu ya kuhamasisha wadau mbalimbali  jinsi ya kudhibiti matumizi ya mihandarati, Mwenyekiti wa muungano huo Silas David na Mwenyekiti wa muungano huo tawi la Vihiga, Alexander Libuha, walisisitiza umuhimu wa kupitishwa kwa sheria inayopendekezwa bungeni ili kuweka adhabu kali kwa wale wanaosambaza mihadarati shuleni wakilenga wlimu na wanafunzi.

Ripoti ya hivi punde kutoka NACADA inaonyesha kuwa asilimia 16.9 ya wanafunzi wa shule za msingi wanatumia dawa za kulevya, wakiwemo asilimia 3.2 wanaovuta tumbaku, asilimia 2.6 wanaokunywa pombe, na asilimia  2.3 wanaotafuna miraa au muguka.

NACADA insema chanzo kikuu cha dawa hizi ni maduka madogo yaliyo karibu na shule na hata ndani ya shule hizo yakichangia (28.6%), baa (25.7%), marafiki (19.3%), wanafunzi wenzao (13.7%), na hata wafanyakazi wa shule (13.6%).

Aidha, wazazi wanahofia idadi kubwa ya walimu waraibu wa mihadarati na pombe wakionekana kuwa mfano mbaya kwa wanafunzi.

Carolyn Necheza
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *