Wingu la majonzi limetanda katika kijiji cha Kiriko kaunti ya Laikipia kufuatia vifo vya watoto wawili wa kike wa miaka nne na moja walioteketea kiasi cha kutotambulika kufuatia mkasa wa moto uliozuka kwa nyumba yao ya familia usiku wa alhamisi.
Kufuatia hali hiyo, majirani wamewaomba wahisani kujitokeza na kusaidia familia hiyo, “wakubwa wetu watusaidie,kwa sababu hawa watu nguo na chakula imechomeka, hivyo tunaomba mtusaidie, musaidie hii nyumba kwa sababu hata sahi wanalala nje.”
Mwengine aliongeza, “yule atakayesikia hili janga ahisi kama yeye ni wa hii familia na aje asaidie.”
Miili hiyo, ilipelekwa kwenye hifadhi ya wafu ya Nyahururu.
Kwengineko, polisi wanachunguza kisa cha mlipuko wa gesi kwenye duka la biashara mjini Oyugis kaunti ya Homabay uliosababisha kifo cha papo hapo cha mwanamume wa umri wa makamo aliye gongwa na mtungi huo huku mwengine akijeruhiwa.
Kwa mujibu wa chifu wa eneo hilo Emily Owor, aliyejeruhiwa alipelekwa hospitalini, akatibiwa kisha akarejeshwa nyumbani.