Wawili wafariki kufuatia ajali ya ndege eneo la Kedong, Naivasha

Martin Mwanje
1 Min Read
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea eneo la Mbaruk kutokea uwanja wa Wilson ajali hiyo ilipotokea / Picha ni kwa hisani ya The Kenya Times

Watu wawili wamefariki kufuatia ajali ya ndege iliyotokea jana Alhamisi, majira ya saa 11:14 jioni, katika eneo la Kedong mjini Naivasha. 

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kenya (KCAA) inasema ndege iliyoanguka ni aina ya Cessna 185 (5Y-BVL).

Kwenye taarifa, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Emile Arao alisema ndege hiyo ilikuwa ikielekea eneo la Mbaruk kutokea uwanja wa Wilson ajali hiyo ilipotokea.

Kulingana na KCAA, kutokea kwa ajali hiyo kuliripotiwa na raia kwa Kituo cha Uratibu wa Uokozi (RCC).

Mamlaka hiyo inasema inafanya kazi na taasisi husika ikiwa ni pamoja na Idara ya Uchunguzi wa Ajali za Ndege (AAID) na maafisa wa usalama wa eneo hilo kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *