Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amekabidhi makundi ya usimamizi wa masuala ya baharini katika kaunti ya kwale boti 19 za kisasa bila malipo ili kuendeleza shughuli za uvuvi baharini hasa katika maji makuu.
Makundi 19 ya kijamii yaliyopokea boti za kisasa ni kutoka maeneo ya Tsunza Kinango, Matuga, Msambweni na LungaLunga kwa gharama ya shilingi milion 58
Boti hizo zinalenga kuongezea wavuvi kutoka ukanda wa kusini mwa pwani mapato ambapo samaki wanaovua wataongezeka kutoka kilo 5 hadi tani 1 kila siku kutokana na uvuvi katika maji makuu.
Mabaharia 76 wakiwemo wanawake 4 walipokea mafunzo na vyeti vya Unahodha na usalama wa baharini kutoka kwa serikali ya Kaunti ya Kwale na shirika la kemfsed
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kwamba shughuli za uvuvi zinaendeshwa katika njia salama na kuepuka majanga baharini.
Kulingana na Gavana Fatuma Achani utoaji wa boti hizo pamoja na utoaji wa vyeti vya Unahodha unalenga kuimarisha sekta ya uchumi samawati ili kutoa nafasi za kutosha za ajira kwa vijana
Viongozi wengine nao walihimiza vijana kuzamia masuala ya baharini ili kujiondoa kwenye lindi la ukosefu wa ajira.