Wachuuzi wa zao la miraa mjini Marsabit waliandamana jana Jumatatu mjini Marsabiti wakitaka usimamizi wa manispaa ya mji huo kuwapa sehemu ya kuendeshea biashara zao.
Wafanyabiashara hao wanadai kukosa maeneo ya kuuzia bidhaa hiyo licha ya kulipa ushuru.
Baadhi ya waliozungumza na wanahabari wamekiri kupitia changamoto kubwa hususan wakati huu wa mvua.
Wameapa kuendelea na maandamano yao kila wiki hadi matakwa yao yatekelezwe.