Watu zaidi ya milioni 54 upembe wa Afrika wanahitaji msaada

Tom Mathinji
1 Min Read

Watu zaidi ya milioni 54 katika eneo la upembe wa Afrika wanahitaji msaada kwa dharura huku athari za mabadiliko ya tabia nchi zikiendelea kudhihirika.

Akiongea kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la maafisa wa ngazi za juu kuhusu kukabiliana na hatari na wadudu waharibifu, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Shirika la IGAD kuhusu ubashiri wa hali ya hewa Dkt. Gulleid Artan alisemahali ya hewa inayoendelea kubadilika pamoja na tishio la wadudu waharibifu wanaovamia mataifa mbalimbali kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ni changamoto kuu inayokabili eneo la upembe wa Afrika.

Alisema kufuatia ubashiri wa kujiri kwa mvua ya El Nino, nchi zote wanachama zinafaa kuchukua hatua za kuzikinga jamii zinazokabiliwa na hatari dhidi ya athari zinazotokana na mvua kubwa.

Katibu wa kilimo anayesimamia ustawi wa mimea Josephat Muhunyu, alitoa wito kwa jamii za wafugaji wa kuhamahama kutekeleza kilimo na ufugaji kwa pamoja ili kuhakikisha wanahimili athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *