Watu wawili wakamatwa wakisafirisha Ethanol

Tom Mathinji
1 Min Read
Malori mawili yanaswa yakisafirisha Ethanol.

Maafisa wa polisi wa idara ya makosa ya Jinai, DCI, waliokuwa wakishika doria katika barabara ya Nakuru-Nairobi, wamewakamata watu wawili wakisafirisha kemikali aina ya ethanol.

Baada ya kupashwa habari, maafisa hao walifanya operesheni na kunasa malori mawili yaliyokuwa yamebeba ethanol, na kufanikiwa kumkamata dereva mmoja huku mwenzake akitoroka.

“Baada ya kupashwa habari kuhusu malori mawili yaliyokuwa yakisafirisha ethanol yenye nambari za usajili KBJ 745M na KAK 903S kutoka Mai Mahiu kuelekea  Nairobi, maafisa wa usalama wa asasi mbali mbali, walianzisha msako na kuyapata yameegeshwa katika eneo la Kamiruthu, Limuru,” ilisema taarifa ya DCI kupitia mtandao wa X.

Hata hivyo dereva mmoja Edward Nandwa, alifanikiwa kutoroka, huku mwenzake Otundo,akikamatwa.

Dereva aliyekamatwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha  Capital Hill, akisubiri kufikishwa mahakamani.

huku malori hayo yako chini ya ulinzi wa polisi.

TAGGED:
Share This Article