Watu wawili wafariki katika ajali ya barabarani Kikuyu

Tom Mathinji
1 Min Read

Watu wawili wamefariki katika ajali ya barabarani huku wengine 10 wakijeruhiwa, katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi ya kampuni ya Eldoret Express na lori la kusafirisha mafuta katika eneo la Muguga, Kikuyu

Akithibitisha ajali hiyo iliyotokea Leo Jumamosi asubuhi, kamanda wa polisi Ronald Kirui, alisema basi hilo lililokuwa na abiria 62, liligonga Lori hilo la kubeba mafuta lililokuwa limesimana saa kumi na moja asubuhi.

Kulingana na  kamanda huyo, miili ya waliofariki ilipelekwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali ya Thogoto, huku magari hayo mawili yakipelekwa katika kituo cha polisi cha Kikuyu.

Afisa huyo mkuu wa polisi ametoa wito kwa Madereva kuwa majini zaidi hasaa wakati huu wa msimu wa mvua.

Ajali hiyo imetokea huku Waziri wa uchukuzi na barabara Kipchumba Murkomen akisema serikali inajizatiti kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani hapa nchini.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article