Watu wawili wafariki baada ya Mgodi kuporomoka Migori

Tom Mathinji
1 Min Read
Wachimbaji Migodi wafariki Migori.

Watu wawili wamefariki baada ya kuta za mgodi wa kina cha mita 750, kuporomoka eneo la Rongo kaunti ya Migori.

Wachimba migodi 18 walikuwa kazini, wakati kuta za mgodi huo zilipoporomoka.

Zaidi ya watu 10 wangali wamekwama ndani ya mgodi huo, huku shuguli za kuwaokoa zikiendelea.

Watu wengine wanne wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Rongo.

Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Rongo, amethibitisha kisa hicho, huku akitoa wito wa msaada zaidi katika shughuli za uokoaji.

Kisa hiki cha Migori, kinajiri wiki moja tu baada ya wachimbaji saba wa migodi kupoteza maisha yao, baada ya mgodi wa Kasweto kilichoko kijiji cha Lumba, kaunti ndogo ya Rarieda kuporomoka.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *