Watu wanne hawajulikani waliko baada ya jengo kuanguka Uthiru

Tom Mathinji
1 Min Read
Jengo laporomoka Uthiru kaunti ya Nairobi.

Watu wanne hawajulikani waliko baada ya jengo la orofa tano kuanguka Jumanne jioni, katika mtaa wa Uthiru kaunti ya Nairobi.

Kulingana na serikali ya kaunti ya Nairobi, maafisa wa kukabiliana na dharura wamefika katika eneo la mkasa na shughuli za uokoaji zinaendelea.

Kupitia kwa taarifa iliyotiwa saini na afisa anayesimamia dharura katika kaunti hiyo Bramwel Simiyu, wanne hao ni pamoja na yaya na watoto wawili kutoka nyumba moja,  na msichana wa umri wa miaka 10 kutonka nyumba nyingine.

“Shughuli za uokoaji zinaendelea na serikali ya kaunti ya Nairobi imepeleka vifaa spesheli kufanikisha shughuli za uokoaji,” alisema Simiyu.

Awali shirika la msalaba mwekundu Kupitia mtandao wake wa X, lilisema limewatuma maafisa wake kusaidia katika shughuli za uokoaji.

Tutakuletea habari zaidi zinapotufikia..

Share This Article