Maafisa wa polisi kutoka idara ya upelelezi wa maswala ya Jinai DCI, wamewakamata watu watatu wakiwa na mbolea ya bei nafuu kinyume cha sheria katika kaunti ya TransNzoia.
Kupitia kwa taarifa ya polisi Leo Jumanne, washukiwa hao walipatikana na magunia 739 ya aina mbali mbali za mbolea ya gharama nafuu, baada ya maafisa hao kufanya msako katika duka moja, linalomilikiwa na Ali Abdi Fatah, eneo la Transnzoia Magharibi.
Washukiwa waliokamatwa katika msako huo ni Ali Abdi Fatah mwenye umri wa miaka 41, na Abdi Jabar Hussein mwenye umri wa miaka 19 wote wawili wa asili ya Somalia na Bonface Awili mwenye raia wa Kenya umri wa miaka 53.
Watatu hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha kitale wakisubiri kufikishwa mahakamani
Mbolea hiyo imehifadhiwa katika ghala la halmashauri ya nafaka na mazao NCPB tawi la kitale