Watu watatu wafariki baada ya jengo kuporomoka Kibra

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu watatu wajeruhiwa baada ya jengo kuporomoka Kibra.

Watu watatu wamefariki baada ya jengo lililokuwa likijengwa kuporomoka katika eneo la Kibra, Jijini Nairobi.

Kulingana na ripoti kutoka kwa kundi la asasi mbali mbali linaloongoza shughuli za uokoaji, watu wengine watatu wameokolewa na wanapokea matibabu katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

Shughuli za uokoaji zinaendelea, zikitekelezwa na maafisa wa polisi, wale serikali ya kaunti ya Nairobi,maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu na kitengo cha kitaifa cha kukabiliana na majanga.

“Jengo limeporomoka katika mtaa wa Highrise eneo la Kibra. Makundi ya dharura yanatekeleza shughuli za uokoaji,” ilisema taarifa kutoka kwa Shirika la Msalaba Mwekundu.

Shirika la Msalaba Mwekundu lilisema watu kadhaa wanahofiwa wamekwama kwenye vifusi vya jengo hilo.

TAGGED:
Share This Article