Watu wasiopungua 53 wafariki kufuatia tetemeko la ardhi eneo la Tibet, China

Martin Mwanje
1 Min Read
Nyumba kadhaa zimeharibika kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea eneo la Tibet nchini China

Watu 53 wamethibitishwa kuaga dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea eneo la Tibet nchini China. 

Mamlaka za nchi hiyo zinasema tetemeko hilo lilikuwa la ukubwa wa 6.8 kwenye kipimo cha Richter.

Vyombo vya habari vya serikali nchini China vinaripoti kuwa nyumba kadhaa zimeanguka karibu na kitovu cha tetemeko hilo lilitokea majira ya saa 3:05 leo Jumanne asubuhi katika kaunti ya Dingri inayopakana na nchi jirani ya Nepal.

Vyombo hivyo vinasema eneo lililopo karibu na kitovu cha tetemeko hilo la ardhi lipo takriban mita 4,000 kwenye mwinuko na linafahamika kama kivutio cha watalii.

Hadi kufikia mwaka 2021, eneo hilo lilikadiriwa kuwa na takriban watu 60,000.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *