Watu sita wafariki kwenye ajali barabarani Nakuru

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu sita wamefariki kwenye ajali barabarani  leo Jumatatu alfajiri  katika eneo la Ngata, kaunti ya Nakuru baada ya lori na matatu  kugongana uso kwa uso.

Kulingana na kamanda wa polisi wa kaunti ya Nakuru Samuel  Ndanyi, ajali hiyo ilitokea majira ya saa tisa alfajiri katika barabara kuu ya Eldoret-Nakuru, wakati dereva wa lori alipopoteza mwelekeo na kugonga gari la abiria 11 ambalo lilikuwa safarini kutoka Kitale kuelekea Nairobi.

Watu sita akiwemo dereva wa gari hilo la abiria walifariki papo hapo huku dereva wa lori akichana mbuga.

Share This Article