Watu milioni 7 nchini DRC watoroka makazi kutokana na ghasia

Tom Mathinji, BBC and BBC
1 Min Read
Watu watoroka makwao katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Umoja wa Mataifa unasema rekodi ya watu milioni 6.9 sasa ni wakimbizi wa ndani kwa ndani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kutokana na kuongezeka kwa ghasia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji limekusanya data za ufuatiliaji kutoka majimbo yote 26 ya nchi hiyo.

Inasema idadi kubwa ya waliokimbia makazi yao wanaishi mashariki ambako migogoro inatajwa kuwa sababu kuu.

Katika eneo la Kivu Kaskazini pekee, takriban watu milioni moja wamekimbia makazi yao mwaka huu, kutokana na mapigano yanayoendelea na waasi wa M23.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa DR Congo inakabiliwa na mojawapo ya matatizo makubwa zaidi ya watu waliokimbia makazi yao na ya kibinadamu.

Website |  + posts
Share This Article