Watu maarufu waliomuunga mkono Trump katika kampeni kuhudhuria uapisho wake

Rais Trump ataapishwa kwa kipindi cha pili uongozini Januari 20, 2025.

Marion Bosire
1 Min Read

Wasanii na watu maarufu ambao walimuunga mkono Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita, wamealikwa kuhudhuria hafla ya kumwapisha.

Orodha hiyo ya watakaohudhuria uapisho wa pili wa Trump inajumuisha wanariadha, washawishi wa mitandaoni, watangazaji wa mitandaoni na wahusika wa vipindi vya hali halisi.

Logan na Jake Paul, Theo Von, Dana White, Amber Rose, Caitlyn Jenner, The Nelk Boys, Bryce Hall na Megyn Kelly ni sehemu ya walio kwenye orodha hiyo.

Inaripotiwa kwamba kuna watu wengine maarufu ambao walikataa mwaliko wa kuhudhuria hafla hiyo kama vile Dr. Phil ambaye ameamua kusalia Texas siku hiyo na kuangazia hafla hiyo mubashara kwenye runinga yake ya Merit.

Wengine ni waigizaji Roseanne Barr, Savannah Chrisley na Drea de Matteo.

Mwimbaji Carrie Underwood ataimba wimbo uitwao ‘America The Beautiful’ kwenye hafla hiyo itakayoandaliwa Januari 20, 2025.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *