Watu kumi wamefariki mapema Jumanne nchini Malasyia kufuatia ajali ya ndege mbili za kijeshi zilizogongana.
Wanajeshi hao walikuwa wakifanya mazoezi ya kijeshi wakati ndege hizo mbili zilipogangana na kuanguka .
Ndege moja ilikuwa na abiria saba huku nyingine ikiwa na abiria watatu na wote wameripotiwa kuaga dunia, huku miili yao ikipelekwa hospitalini kutambuliwa.
Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo.