Watu kadhaa wanahofiwa kunaswa ndani ya jengo la orofa 22, lililoporomoka mtaani Westlands, kaunti ya Nairobi Jumatano jioni.
Watu hao wanaaminika kuwa wajenzi wa orofa hiyo ambayo sehemu yake iliporomoka.
Taarifa kutoka kwa shirika la msalaba mwekundu ilisema kuwa shughuli ya uokozi ingali inaendelea kwenye vifusi vya jengo hilo.
Watu wawili kati ya wanne waliokuwa ndani ya jengo hilo walinusurika bila majeraha na kufanikiwa kuhep,a huku wengine wawili wakiaminika kunaswa ndani yake.