Watu kadhaa wanahofiwa kufariki huku wengi wakijeruhiwa vibaya kwenye ajali ya barabarani iliyohusisha gari la matatu katika kaunti ya Machakos Jumatatu jioni.
Kulingana na kamanada wa polisi wa kaunti ndogo ya Yatta Jane Makau watu wanane walifariki papo hapo katika ajali hiyo iliyotokea katika barabara ya Katangi-Machakos-Kitui-Nairobi kilomita kadhaa kutoka daraja la mto Athi,
Majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa katika hospitali ya Machakos Level 5 kwa matibabu.
Gari hilo lililokuwa na magunia kadhaa ya makaa lilipoteza mwelekeo na kutumbukia katika shimo.
Ajali hiyo ilihusisha matatu ya watu 42 iliy0kuwa likisafiri kutoka kKtui kuelekea na kuanguka.